voaswahili images

Discover Best voaswahili Images of World

#food #travel #sports #news #april #saturday

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd J Austin amezungumza na Waziri wa Baraza la Mawaziri (CS) wa Ulinzi, Aden Dual kutuma salaam za rambi rambi kwa kifo cha Mkuu wa Majeshi ya Kenya, Jenerali Francis Ogolla na wanajeshi wengine tisa kwa ajili ya helikopta ya jeshi April 18. Bwana Duale alimuelezea Jenerali Ogolla kuwa ni kiongozi anayeheshimiwa sana ambaye alifanya kazi kwa bidi kuhakikisha ushirikiano wa ulinzi wa Marekani na Kenya ni imara. Kwa mujibu wa msemaji wa Pentagon Meja Jenerali Pat Ryder, Dual alielezea shukrani zake kwa simu ya Waziri Austin.⁣⁣ #waziri #ulinzi #LloydAustin #barazalamawaziri #kenya #marekani #francisogolla #jenerali #adendual #nairobi #voa #voaswahili

4/20/2024, 7:46:42 AM

Bassirou Diomaye Faye ameapishwa kuwa Rais wa Taifa la Senegal huko Diamniadio karibu na mji mkuu wa Dakar, leo Aprili 02, 2024. Diomaye amekabidhiwa rasmi madaraka na rais anayeondoka madarakani Macky Sall, kuwa Rais wa Tano wa Taifa la Senegal tangu Nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1960. #acd_habariupdates #kiwandachahabari #tunakufahamishausiyoyafahamu #wasafimedia #wasafi #wasafitv #wasafifm #millardayoupdates #sénégal #itv #voa #voaswahili

4/2/2024, 9:00:35 PM

Rais Joe Biden akitoa hotuba yake ya tatu ya Hali ya Kitaifa na pengine yenye kishindo kikubwa akiwa ana matumaini ya kuuza kwa umma wa Wamarekani azma ya kuendelea na muhula wa pili.⁣⁣⁣ ⁣Biden amekusudia kutumia hotuba yake kuwahimiza wapiga kura kukataa "simulizi zilizoko Marekani za kinyongo, kuadhibu, na kulipiza kisasi" wakati alipokuwa akiwasilisha hoja yake kwa wapiga kura waliovunjika moyo na kuonya kuwa mgombea anayeongoza uchaguzi wa Chama cha Republikan atakuwa ni chaguo mbadala hatari. (AP/VOA) ⁣⁣⁣ ⁣⁣⁣ ⁣⁣⁣ #sotu #biden #voaswahili

3/8/2024, 7:26:45 PM

Rais Joe Biden akitoa hotuba yake ya tatu ya Hali ya Kitaifa na pengine yenye kishindo kikubwa akiwa ana matumaini ya kuuza kwa umma wa Wamarekani azma ya kuendelea na muhula wa pili.⁣⁣⁣ ⁣Biden amekusudia kutumia hotuba yake kuwahimiza wapiga kura kukataa "simulizi zilizoko Marekani za kinyongo, kuadhibu, na kulipiza kisasi" wakati alipokuwa akiwasilisha hoja yake kwa wapiga kura waliovunjika moyo na kuonya kuwa mgombea anayeongoza uchaguzi wa Chama cha Republikan atakuwa ni chaguo mbadala hatari. (AP/VOA) ⁣⁣⁣ ⁣⁣⁣ ⁣⁣⁣ #sotu #biden #voaswahili

3/8/2024, 9:43:32 AM

Rais Joe Biden akitoa hotuba yake ya tatu ya Hali ya Kitaifa na pengine yenye kishindo kikubwa akiwa ana matumaini ya kuuza kwa umma wa Wamarekani azma ya kuendelea na muhula wa pili.⁣⁣ ⁣Biden amekusudia kutumia hotuba yake kuwahimiza wapiga kura kukataa "simulizi zilizoko Marekani za kinyongo, kuadhibu, na kulipiza kisasi" wakati alipokuwa akiwasilisha hoja yake kwa wapiga kura waliovunjika moyo na kuonya kuwa mgombea anayeongoza uchaguzi wa Chama cha Republikan atakuwa ni chaguo mbadala hatari. (AP/VOA) ⁣⁣ ⁣⁣ ⁣⁣ #sotu #biden #voaswahili

3/8/2024, 9:07:45 AM

KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA IVORY COAST 2023: ROUNDI YA 16⁣ #AFCON #IvoryCoast #football #senegal #cameroon #equatorialguinea #ivorycoast #voa #voaswahili #mchezo #raundiya16

1/28/2024, 9:42:59 PM

Ukraine Alhamisi imesema ilitungua ndege 11 zisizokuwa na rubani za Russia kati ya 14 zilizotumiwa na jeshi la Russia usiku kucha na kujeruhi watu kadhaa katika mikoa ya kusini ya bahari ya Black Sea. Kyiv iliwaomba washirika wake wa nchi za Magharibi kuimarisha mifumo yake ya ulinzi wa anga, huku Moscow ikiendelea na mashambulizi yake ya usiku kucha kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani na makombora kwenye miji na miundombinu muhimu kote nchini Ukraine. Wizara ya mambo ya ndani imesema mashambulizi hayo yalijeruhi watu sita katika mji wa kihistoria wa Odesa na kuharibu majengo ya makazi ya watu na ghala.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #ukraine #russia #drone #putin #zelenskyy

1/25/2024, 6:49:16 PM

Afisa muandamizi wa Umoja wa Mataifa Alhamisi ametoa wito wa “kuchukuliwa kila hatua” kuwalinda raia, kufuatia shambulio ambapo watu 12 waliuawa wakati kituo cha mafunzo cha Umoja wa mataifa kinachohifadhi maelefu ya Wapalestina waliohama makazi yao kiliposhambuliwa kwa mizinga iliyofyetuliwa na kifaru. Thomas White, mkurungenzi wa masuala ya Gaza kwenye shirika la Umoja wa Mataifa UNRWA, amesema hali huko Khan Younis, mji wa kusini mwa Gaza ambako shambulio hilo lilitokea, unadhihirisha kushindwa kabisa kuheshimu kanuni za msingi za sheria ya kimataifa wakati wa vita.⁣ Jeshi la Israel limesema haliamini shambulio hilo la mizinga lilifanywa na wanajeshi lakini limesema tukio hilo linafanyiwa uchunguzi. Limesema pia eneo kubwa la Khan Younis ni ngome muhimu kwa wanamgambo wa Hamas.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #gaza #ukanda #un #hamas #israel

1/25/2024, 6:42:25 PM

Shirika la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch Alhamisi limelishtumu jeshi la Burkina Faso kuua takriban raia 60 katika mashambulizi ya ndege isiyokuwa na rubani ambayo serikali ilisema ilikuwa inawalenga wanamgambo wa kiislamu. Human Rights Watch imesema katika ripoti yake kwamba Vifo hivyo vilitokea katika mashambulizi matatu ya ndege isiyokuwa na rubani tangu Agosti, mawili kwenye masoko yenye watu wengi na jingine katika mazishi.⁣ Kiongozi wa kijeshi Kepteni Ibrahim Traore ambaye aliingia madarakani baada ya mapinduzi ya 2022, amelilipa kipaumbele suala la usalama kwa kutumia nguvu kali kukabiliana na mashambulizi ya makundi yenye uhusiana na makundi ya kigaidi ya Al-Qaeda na Islamic State. Human Rights Watch imesema iliwahoji watu kadhaa na mashahidi kati ya mwezi Septemba na Novemba na ilichunguza picha, video na picha za satellite.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #burkinafaso #Traore #drone

1/25/2024, 6:36:39 PM

Wajumbe Israel na Hamas wamefikia karibu na makubaliano ya sitisho la mapigano katika ukanda wa Gaza na kuachiliwa mateka wa Israel na wafungwa wa Palestina. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, hayo yanajiri wakati ambapo Israel inaendelea na mashambulizi yake makubwa ya mwezi huu kusini mwa Gaza. Qatar, Marekani na Misri zimekuwa zikiongoza juhudi za upatanishi kati ya pande zote kwa wiki kadhaa juu ya kuachiliwa mateka kwa mabadilishano ya kusitisha mapigano, kuachiliwa wafungwa wa Palestina na misaada zaidi katika kanda hiyo. Lakini mpango huo umezuiwa, vyanzo vya habari vimesema kutokana na kwamba Hamas na Israel wana tofautiana juu ya jinsi ya kumaliza kabisa vita katika ukanda wa Gaza.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #israel #gaza #marekani #misri #qatar

1/24/2024, 6:18:04 PM

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amepata ushindi katika jimbo la New Hampshire Jumanne kupitia chama chake cha Republican hatua inayomsogeza karibu kuchuana tena katika uchaguzi mwezi Novemba na rais Joe Biden hata wakati ambapo mpinzani wake pekee aliyebaki Nikki Haley kuahidi kuendelea kupambana. Wachambuzi wa kisiasa wanasema Haley anakabiliwa na ushindani mkubwa katika uchaguzi wa awali unaoelekea katika jimbo la nyumbani kwake south carolina ambako alikuwa gavana, lakini ni jimbo ambalo Trump ana uungwaji mkono mkubwa. ⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #marekani #trump #biden #haley #newhampshire

1/24/2024, 6:12:01 PM

Mazishi yalifanyika mjini Jerusalem kwa ajili ya Luteni Hadar Kapluk, mmoja kati ya wanajeshi 24 wa Israel waliouawa katika Ukanda wa Gaza. Vifo vya wanajeshi hao vimetajwa kuwa shambulio mbaya zaidi dhidi ya wanajeshi wa Israel tangu mashambulizi ya ardhini ya nchi hiyo huko Gaza kuanza mwishoni mwa Oktoba. Idara ya ulinzi imesema kuwa guruneti lililofyetuliwa na roketi kwenye kifaru lilisababisha mlipuko wa pili ulioangusha majengo mawili kwa wanajeshi hao.⁣ ⁣ Msemaji wa jeshi la Israel Daniel Hagari amesema vita vina gharama chungu sana na nzito na kuwataja wanajeshi hao wa akiba waliojitolea kutetea bendera kuwa walifanya hivo kwa ajili ya Taifa la kwa ajili ya usalama wa taifa.⁣ Aidha kwa upande wake Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ameapa kusonga mbele hadi Israel itakapoliangamiza kundi la wapiganaji wa Hamas na kupata uhuru wa mateka zaidi ya 100 wanaoshikiliwa huko Gaza. Idadi hiyo kubwa ya vifo inaweza kuongeza juhudi mpya ya kuitaka Israel kusitisha mashambulizi au hata kusitisha vita kabisa.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #israel #gaza #hamas #netanyahu⁣ ⁣

1/23/2024, 7:59:22 PM

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anakutana na Marais wa Nigeria na Ivory Coast katika jitihada za kuunda mshikamano na mataifa hayo mawili muhimu ya kidemokrasia barani Afrika wakati mizozo ikiikumba dunia.⁣ Mjini Abidjan, Blinken alikutana na Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara, kiongozi mkongwe ambaye amepata sifa za Marekani kwa kuimarisha demokrasia, kabla ya kuelekea Abuja kumuona Rais wa Nigeria Bola Tinubu, aliyechaguliwa mwaka jana. Blinken, wakati wa mkutano na waandishi wa habari na Rais Ouattara, aliipongeza Ivory Coast kwa uongozi wake katika kukabiliana na itikadi kali na ghasia.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #marekani #blinken #nigeria #ivorycoast ⁣ ⁣

1/23/2024, 7:53:49 PM

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken wiki ijayo atayatembelea mataifa manne ya Cape Verde, Ivory Coast, Nigeria, na Angola wiki ijayo, wizara hiyo imesema katika taarifa yake. Hii ni ziara yake ya nne katika bara hilo. Ziara hiyo inakuja baada ya ile ya mwaka jana ya maafisa 17 wa ngazi ya mawaziri, ikiwa ni kufuatilia mkutano wa viongozi wa Marekani na Afrika uliofanyika Washington 2022. Waziri mdogo wa mambo ya nje wa kwa masuala ya Afrika, Molly Phee amesema wakati mashindano ya kandanda ya mataifa ya Afrika (AFCON) yakiendelea, Blinken ana matumaini ya kuhudhuria mechi wakati akiwa nchini Ivory Coast.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #africon #marekani #biden #blinken #ivorycoast

1/19/2024, 8:49:52 PM

Viongozi wa nchi zisizofungamana na upande wowote (NAM) siku ya Ijumaa wamelaani kampeni ya kijeshi ya Israel huko Gaza na kutaka usitishaji wa mapigano hayo mara moja, wakati wa mkutano wa kila mwaka wa wajumbe 120 wa jumuiya hiyo. Dazerni ya wakuu wa nchi na maafisa waandamizi kutoka NAM, iliyoundwa rasmi mwaka 1961 na nchi zilizopinga kujiunga na upande wowote wa kambi kuu mbili wakati wa enzi ya vita baridi wanahudhuria mkutano unaofanyika kampala, Uganda.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #nam #uganda #coldwar #vitabaridi #gaza #israel #hamas

1/19/2024, 8:32:03 PM

Afisa wa ngazi ya juu wa kundi la kigaidi la ki-Houthi linaloungwa mkono na Iran amesema meli za China na Russia zitakuwa na njia salama kupitia bahari ya Sham. Mohammed al-Bukhaiti, mwanachama wa uongozi wa kisiasa wa ki-Houthi, alisema katika mahojiano na kituo cha Russia cha Izvestia kwamba njia za meli zinazozunguka Yemen ni salama kwa meli kutoka China na Russia, mradi tu meli hazihusiani na Israeli, Agence France-Presse iliripoti Ijumaa, ikinukuu Izvestia. Wa-houthi wamesema wanafanya kazi kwa mshikamano na Wa-palestina kufuatia vita vya Israel dhidi ya wanamgambo wa Hamas huko Gaza, na wamefanya mashambulizi zaidi ya 30 katika Bahari ya Sham. Hata hivyo, Wa-houthi wameanzisha mashambulizi dhidi ya meli ambazo hazina uhusiano wowote na Israel, na kusababisha baadhi ya makampuni ya meli kuepuka njia za meli ambako Wa-houthi wameanzisha mashambulizi.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #houthi #iran #china #russia #shamu #redsea

1/19/2024, 6:47:24 PM

Kanda za nadra ambazo taasisi ya wataalam ya Korea Kusini ilizipata zilionyesha wanafunzi wawili wa shule ya sekondari wenye umri wa miaka 16 huko Korea Kaskazini wakihukumiwa kifung cha miaka 12 jela na kazi ngumu kwa kutazama na kuzisambaza filamu na tamthilia za Korea Kusini. Katika video hiyo, ambayo Reuters haiwezi kuthibitisha kutoka vyanzo huru, wanafunzi hao wawili waliweza kuonekana wakiwa wamesimama kwenye kesi mbele ya mamia ya wenzao.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #korea #kusini #kaskazini #uhuru #dikteta #kimjongun

1/19/2024, 6:38:33 PM

Iran imesema Ijumaa kuwa imefanikiwa kufanya mazoezi ya ulinzi wa anga kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani zilizobuniwa kuzuia silaha za adui katika eneo linaloanzia pwani yake ya kusini magharibi hadi kusini mashariki, huku kukiwa na hali ya wasiwasi katika kanda hiyo. Siku ya Alhamisi Pakistan ilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya kile ilichosema ni wanamgambo wanaotaka kujitenga ndani ya Iran katika shambulio la kulipiza kisasi, siku mbili baada ya Tehran kusema kuwa ilishambulia kambi za kundi jingine ndani ya ardhi ya Pakistan. ⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #iran #pakistani #israel

1/19/2024, 6:28:50 PM

Ghasia za baada ya uchaguzi nchini Comoro zimekuwa mbaya siku ya Alhamisi wakati mtu wa kwanza kufariki baada ya kupigwa risasi, huku wanajeshi wakipambana na waandamanaji katika mitaa ya mji mkuu wa Moroni. ⁣ Mkuu wa chumba za dharura katika hospitali ya El Maarouf iliyoko, Moroni, Dr Djabir Ibrahim aliwaambia waandishi wa habari kuwa watu sita wamejeruhiwa na wamelazwa hospitali na kijana mwenye umri wa miaka 21 amefariki, “uwezekano mkubwa kwa kupigwa risasi”⁣ Akikaidi mvua nyingi na mabomu ya kutoa machozi kijana, mwenye umri wa miaka 20 hivi, akiwa amefunika uso wake aliliambia shirika la habari la AFP siku ya Alhamisi ni kwa nini ghasia zimezuka tena katika visiwa hivyo kwenye Bahari ya Hindi. “Tumekuwa tukipigana kwa zaidi ya saa 24 kwa sababu hatukubaliani na matokeo ya uchaguzi. Ndiyo maana tunachoma majengo ya serikali.”⁣ Vijana wamekuwa wakijaribu kuweka vizuizi barabarani na mitaani katika mji kuu wa Moroni, wakiwatupia mawe maafisa wa usalama, ambao wamekuwa wakijaribu kuwatawanya lakini vijana wamekuwa wakikimbilia vichochoroni na kuwasubiri.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #comoro #uchaguzi #upinzani #assoumani, ⁣

1/18/2024, 7:07:09 PM

Jeshi la Ukraine limeripoti Alhamisi kutungua ndege zisizo na rubani (drone) 22 za Russia kati ya 33 katika mashambulizi ya usiku kucha. Ndege hizo zilikuwa zimeelekezwa Kaskazini na Kusini mwa Ukraine, ikiwemo mikoa ya Sumy, Kherson na Dnipropetrovsk. Nayo wizara ya ulinzi ya Russia imesema mifumo yake ya ulinzi wa anga iliharibu ndege moja isiyokuwa na rubani ya Ukraine juu ya eneo la Moscow, huku nyingine ikinaswa karibu na mji wa pili mkubwa wa Russia, St Petersburg. Meya wa mji wa Moscow Sergei Sobyanin amesema kwenye mtandao wa Telegram kwamba hakuna maafa au uharibifu kutoka kwenye mabaki ya ndege isiyo na rubani iliyotunguliwa.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #ukraine #russia #drone #putin #zelenskyy

1/18/2024, 5:55:17 PM

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda na mgombea wa zamani wa urais Bobi Wine Alhamisi amesema polisi waliizingira nyumba yake na kumuweka “chini ya kizuizi cha nyumbani” kabla ya maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika. Wanasiasa wa upinzani walikuwa wamepanga maandamano dhidi ya barabara mbovu sana nchini Uganda, ambayo ni mwenyeji wa mikutano miwili ya kimataifa katika siku zijazo. Wine, mwanamuziki aliyegeuka kuwa mwanasiasa, amesema polisi na wanajeshi wamemzuia kuondoka nyumbani kwake huko Magere, Kaskazini Magharibi mwa mji mkuu Kampala. Wine, ambaye jina lake la kweli ni Robert Kyagulanyi alishindana na Rais mkongwe Yoweri Museveni kwenye uchaguzi wa mwaka 2021, akiomba kumalizwa kwa utawala wa kimabavu wa Rais Yoweri Museveni.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #bobiwine #uganda #museveni #upinzani #maandamano

1/18/2024, 5:41:37 PM

Pakistan Alhamisi imesema kwamba jeshi lake limefanya mashambulizi dhidi ya “maficho ya magaidi” katika nchi jirani ya Iran, siku mbili baada ya Tehran kushambulia kwa mabomu kile ilichosema kuwa ililenga “magaidi wa Iran” wanaopewa hifadhi kwenye ardhi ya Pakistan. Wizara ya mambo ya nje ya Pakistan imesema kwamba mashambulizi yake ya kijeshi “yaliyopangwa vizuri na yaliyolenga wahusika” yameua magaidi kadhaa katika mkoa wa Sistan-Baluchistan ulioko mpakani na Iran. Chanzo cha usalama ambacho hakikutaka jina lake litajwe kimeiambia VOA kwamba ndege za kivita zilifanya mashambulizi hayo bila kuingia anga ya Iran na kulenga kambi za jeshi la ukombozi la Baluchistan linaloipinga Pakistan au BLA, lililotajwa na Marekani kama kundi la kimataifa la kigaidi.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #pakistani #iran #bla #baluchistan

1/18/2024, 5:28:34 PM

Mashambulizi ya Israel yameua zaidi ya watu 90 usiku kucha, wizara ya afya chini ya utawala wa Hamas huko Gaza imesema siku ya Alhamisi. Mashambulizi hayo mapya yamefanyika huku madawa kwa ajili ya mateka wanaoshikiliwa na wanamgambo na msaada mpya kwa raia ukiingia katika eneo la Palestina chini ya makubaliano mapya ya hivi karibuni, imesema Qatar ambaye ni mpatanishi. Wizara ya afya huko Gaza imesema watu 93 waliuawa, wakiwemo 16 waliouawa katika shambulio moja kwenye nyumba katika mji wa kusini wa Rafah, ambako watu wengi walikimbilia. “Shambulio hilo limeua watu 16, miongoni mwao wanawake na watoto, na wengine 20 walijeruhiwa,” wizara hiyo imesema. Israel imesema mashambulizi yake yamewalenga wanamgambo wa Hamas Kaskazini na Kusini mwa Ukanda wa Gaza.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #gaza #hamas #israel #qatar #misri #marekani

1/18/2024, 5:19:13 PM

Kumbukumbu ya Martin Luther King Jr. ⁣ Marekani yasherehekea Sikukuu ya Martin Luther King Jr. leo Jumatatu kumuenzi mchango wake katika kupigania haki za watu weusi na haki ya kupiga kura. Hii ni moja ya nukuu muhimu aliyoitoa Dkt. King kuhusu kusudio lake la kuweka ushawishi katika sera ya Marekani kuhusu ubaguzi uliokuwepo Afrika Kusini...⁣ #kumbukumbu #kumuenzi #martinlutherkingjr #Marekani #Afrika #voa #voaswahili #hakizakiraia #ubaguzi #sera #AfrikaKusini

1/15/2024, 7:09:51 AM

Kumbukumbu ya Martin Luther King Jr. ⁣ Marekani yasherehekea Sikukuu ya Martin Luther King Jr. leo Jumatatu kumuenzi mchango wake katika kupigania haki za watu weusi na haki ya kupiga kura. Hii ni moja ya nukuu muhimu aliyoitoa Dkt. King kuhusu Ukandamizaji na jinsi ya kupambana nao...⁣ #kumbukumbu #kumuenzi #martinlutherkingjr #Marekani #Afrika #voa #voaswahili #hakizakiraia

1/15/2024, 7:01:47 AM

Biashara kati ya China na Russia mwaka 2023 imeripotiwa kuvunja rekodi kulingana na takwimu rasmi zilizotolewa Ijumaa na Beijing, huku biashara na Marekani ikishuka kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 4, wakati mivutano ya kieneo na kisiasa ikiendelea kuongezeka. Biashara kati ya China na Russia imeripotiwa kufikia zaidi ya dola bilioni 240, kulingana na takwimu za idara ya ushuru, kiwango ambacho kimepita dola bilioni 200 zilizokisiwa na mataifa hayo wakati wa kikao cha pamoja mwaka uliopita.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #china #russia #trade #marekani

1/12/2024, 9:45:24 PM

Japan siku ya Ijumaa imerusha roketi iliyobeba satalaiti ya kijasusi ya serikali, kwa lengo la kuchunguza harakati kwenye vituo vya kijeshi vya Korea Kaskazini, pamoja na kuimarisha uangalizi wa majanga asilia. Chombo hicho aina ya H2A kimerushwa na kampuni ya Mitsubishi Heavy Industries, kutoka kwenye kituo cha anga za juu cha Tanegashima, kusini magharibi mwa Japan, kikiwa kimebeba satellite yenye uwezo wa kupiga picha, kama sehemu ya juhudi za Tokyo za kuimarisha uwezo wake wa kijeshi. Kituo cha Satellite cha serikali pamoja na kampuni ya Mitsubishi wamesema kwamba zoezi hilo limefanyika kwa mafanikio kwa kuwa satellite hiyo aina ya Optical -8 ilitenganishwa na roketi na kuingia kwenye anga za juu kama ilivyopangwa.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #japan #kimjongun

1/12/2024, 9:37:33 PM

Russia imesema kwamba imeitisha kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa, ili kuzungumzia mashambulizi ya kijeshi kwa Yemen kutoka kwa Marekani na Uingereza. Marekani na Uingereza wameanzisha mashambulizi ya anga na baharini dhidi ya malengo ya wahouthi nchini Yemen, ikiwa ni majibu kwa mashambulizi dhidi ya meli kwenye bahari ya Sham, hatua inayoonekana kuenea kikanda kwa vita vya Israel na Hamas huko Gaza. Msemaji wa kundi la kihouthi amesema mashambulizi ya Marekani na Uingereza hayana uhalali, na kwamba kundi hilo linaloungwa mkono na Iran litaendelea kushambulia meli zinazoelekea Israel. Kamandi ya Marekani imesema Alhamisi jioni kwamba mashambulizi hayo yalilenga zaidi ya malengo 60 kwenye maeneo 16 katika eneo linalodhibitiwa na wa Houthi ndani ya Yemen. ⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #russia #ukraine #yemen #uingereza #gaza #israel

1/12/2024, 9:20:45 PM

Kiongozi wa upinani nchini Russia aliye gerezani Alexei Navalny alionekana mbele ya jaji wa mahakama ya juu kwa njia ya video kuwasilisha ombi kudai haki ya muda mrefu zaidi wakati wa chakula na fursa ya kupata vitabu zaidi akiwa gerezani. Akiwa amevaa sare nyeusi ya gerezani na amesimama nyuma ya vyuma, akiwa miguu chini, Navalny mwenye umri wa miaka 47, alionekana akiongea pole pole lakini alizungumza kwa mifano na kwa kirefu na bila ya kusoma popote. Navalny alisema kanuni za magereza zinawapa fursa wafungwa ya kuwa na kitabu kimoja, kwahiyo mfungwa anapoamua kuchukua Biblia au Koran basi hawezi kupewa vitabu vingine vya dini au vyoyote vile, ikiwa ni pamoja na magazeti na majarida.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #russia #navalny #putin #upinzani

1/11/2024, 9:21:14 PM

Makombora mawili ya Russia yamepiga hoteli moja usiku wa Jumatano katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine wa Kharhiv, na kujeruhi watu 11, mtu mmoja akiwa mahututi, Gavana wa mkoa amesema. Timu za dharura zilifanya kazi kwenye mabaki ya jengo hilo ambapo madirisha yalivunjwa na roshani ziliharibiwa na kuwepo kwa kifusi kikubwa mtaani. Gavana wa Kharkiv Oleh Synehubo, akiandika kwenye Telegram, akisema shambulizi limefanyika kiasi cha saa nne na nusu usiku kwa saa za huko na kuhusisha makombora aina ya S-300 katika wilaya ya Kyiv. Mkuu wa polisi wa mkoa wa Kharkiv Volodymyr Tymoshko amesema waandishi wa kiamtaifa walikuwa wakikaa kwenye hoteli hiyo. Mwandishi mmoja wa Uturuki alijeruhiwa, amesema.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #russia #ukraine #putin

1/11/2024, 9:08:32 PM

Msemaji serikali wa Somalia amesema Alhamisi kwamba serikali inafanya kila juhudi ili kuwaokoa abiria waliokuwa katika helikopta ya Umoja wa Mataifa iliyotekwa nyara na wanamgambo wa al Shaabab, ingawa mafisa wa kijeshi wamesema kwamba huenda ikawa vigumu kufika mahala walikopelekwa. Helikopta hiyo iliyokodishwa na UN ilikuwa ikipeleka dawa, wakati hitilafu za kimitambo zilipoilazimisha kutua kwa dharura karibu na kijiji cha Hindhere, kililochoko katikati mwa Somalia, na kinachodhibitiwa na wanamgambo. Wanaume wawili raia wa Somalia pamoja na raia kadhaa wa kigeni ni miongoni mwa watu waliokuwa ndani ya helikopta hiyo, wengi wao walichukuliwa mateka na wanamgambo, maafisa wawili wa usalama wameiambia Reuters.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #un #alshabaab #somalia

1/11/2024, 5:46:40 PM

Majaji kwenye mahakama ya Kimataifa ya Haki Alhamisi wameanza siku mbili za kusikiliza kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini, ikiishutumu Israel kwa kutekeleza mauaji ya kimbari katika vita vyake huko Gaza. Afrika Kusini imeiomba mahakama hiyo iamuru kusitishwa mara moja kwa kampeni ya Israel huko Gaza, ambako Israel imesema kwamba nia yake ni kuliangamiza kundi la Hamas, kufuatia shambulizi la Oktoba 7 kusini mwa Israel. ⁣ Waraka uliowasilishwa na Afrika Kusini unasema kwamba ungependa kuona mahakama hiyo ikiiwajibisha Israel kwa kukikuka mkataba unaopinga mauaji ya halaiki, pamoja na kuhakikisha uwezekano wa ulinzi kamili wa wapalestina waliopo Gaza, ambao wako kwenye hatari kubwa na ya haraka kutokana na kuendelea kwa vitendo vya mauaji ya kimbari. Israel imezipuuza tuhuma hizo kuwa hazina msingi. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Jumatano jioni alisema kwamba vikosi vya Israel vinafanya kila viwezalo kuzuia vifo vya raia, wakati akiwashutumu wanamgambo wa Hamas kwa kutumia raia kama ngao. ⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #makama #hague #israel #afrikakusini #gaza #israel

1/11/2024, 5:29:24 PM

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, Alhamisi anakutana na rais wa Misri Abdel Fattah el Sissi, huku kukiwa na juhudi za kudhibiti vita vya Israel na Hamas huko Ukanda wa Gaza, pamoja na kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na wanamgambo huko Gaza. Misri imekuwa na jukumu kuu katika mashauriano ya awali yaliyopelekea sitisho la muda la mapigano, wakati ambapo Hamas, iliwaachilia zaidi ya mateka 100, huku Israel ikiachilia zaidi ya wafungwa 240 wa kipalestina. ⁣ Jenerali mstaafu wa jeshi Frank McKenzie, aliyewahi kuwa kamanda wa kikosi cha kamandi kuu ya Marekani, Jumatano katika mahojiano kwa njia ya Webinar alielezea wasi wasi wake kuhusu kuachiliwa kwa mateka waliobaki walio mikononi mwa Hamas. Mazungumzo ya Blinken mjini Cairo yanafanyika siku moja baada ya kukutana na rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas, huko Ukingo wa Magharibi, wakati pia Abbas baadaye akikutana na Al Sissi pamoja na mfalme wa Abdullah wa Jordan.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #marekani #bliken #gaza #israel #hamas

1/11/2024, 5:17:20 PM

Wizara ya mambo ya nje China imeeleza kukasirishwa kwake siku ya Jumatano baada ya balozi wa Taiwan nchini Marekani kukutana na spika wa baraza la wawakilishi la Marekani Mike Johnson Jumanne. ⁣ Wabunge wa Marekani wanatakiwa kuacha “kutuma ishara mbaya kwa makundi yanayotaka kujitenga ya Taiwan na wasiingilie katika uchaguzi wa ndani wa Taiwan kwa njia yoyote,” msemaji Mao Ning aliwaambia waandishi wa habari.⁣ Marekani ni muungwaji mkono muhimu wa kimataifa wa Taiwan na muuzaji mkubwa wa silaha licha ya ukosefu wa ushirikiano rasmi wa kidiplomasia na kisiwa hicho ambacho china inakiona ni cha kwake. ⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #china #taiwani #marekani #bunge #diplomasia

1/10/2024, 8:25:07 PM

Iraq inataka majadiliano ya haraka ya kuondoka vikosi vya jeshi vinavyoongozwa na Marekani kutoka katika ardhi yake lakini haijaweka tarehe ya mwisho, waziri mkuu Mohammed Shia al Sudani alisema, akieleza uwepo wao kama unavuruga utulivu wakati kukiwa na wasi wasi kuhusu vita vya Gaza.⁣ Wito wa muda mrefu hasa kutoka makundi waislamu wa Kishia wengi walio karibu na Iran kutaka ushirika unaoongozwa na Marekani kuondoka, umeshika kasi baada ya mfululizo wa mashambulizi ya Marekani dhidi ya makundi ya wanamgambo yenye uhusiano na Iran ambayo pia ni sehemu ya vikosi rasmi vya usalama vya Iraq. Mashambulizi hayo yaliyofanyika ili kujibu darzeni za mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani na makombora kwa vikosi vya Marekani tangu israel ilipoanzisha mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza vimeongeza hofu kuwa Iraq inaweza kurejea tena kuwa kituo cha mizozo ya kikanda. ⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #irag #marekani #shia #gaza

1/10/2024, 8:00:08 PM

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amekutana na mkuu wa Mamlaka wa Palestina Mahamoud Abbas, ambapo Washington inatarajia ataweza kuongoza Gaza baada ya vita vya Israel na Hamas kumalizika. Mwanadiplomasia huyo wa juu wa Marekani yuko katika ziara yake ya nne ya mzozo katika Mashariki ya kati tangu vita katika Ukanda wa Gaza kuzuka. Alikutana pia na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Tel Aviv Jumanne. Blinken aliuambia mkutano na waandishi wa habari kwamba Marekani itaendelea kumuunga mkono mshirika wake lakini pia alitoa wito kwa Israel kufanya juhudi zaidi kulinda wale waliokwama katika kitongoji cha Palestina kilichozingirwa akisema kuwa idadi ya raia walioathiriwa huko Gaza hasa watoto inazidi kuongezeka. Jummane Blinken alisema Israel lazima isitishe kuchukua hatua zinazozuia uwezo wa Palestina kujiongoza yenyewe ipasavyo akisistiza umuhimu wa maendeleo ya kutafuta suluhu ya mataifa mawili.•⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #marekani #blinken #israel #hamas #palestina

1/10/2024, 7:49:25 PM

Misri imekataa pendekezo la Israel la kutaka kuwa mwangalizi mkuu wa eneo lisilo na silaha kati ya mpaka wa Misri na Gaza, na kuzipa kipaumbele juhudi za usimamizi wa sitisho la mapigano kabla ya kushughulikia mipango ya baada ya vita, vyanzo vitatu vya usalama vya Misri vimesema. Misri inashirikiana mpaka wa kilometa 13 na Gaza, ni mpaka pekee uliopo katika pwani ya Palestina ambao haudhibitiwi moja kwa moja na Israel. Pamoja na Qatar, Misri pia ina jukumu la kuongoza mazungumzo katika kusimamia sitisho jipya la mapigano huko Gaza na kufanikisha makubaliano ya kuachiliwa mateka wa Israel wanaoshikiliwa na Hamas. Vyanzo vya Misri vimesema wakati wa mazungumzo hayo Israel iliieleza Misri kuhusu uimarishaji wa njia ya Philadelphi, eneo jembamba lisilo na silaha kwenye mpaka, kama sehemu ya mipango ya Israel kuzuia mashambulizi ya baadaye. Mgogoro wa sasa umeanza Oktoba 7, wakati Hamas ilipoanya uvamizi ambapo Israel imesema watu 1,200 waliuawa na wengine wapatao 240 kuchukuliwa mateka.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #misri #gaza #israel #qatar

1/9/2024, 8:33:00 PM

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken amekutana na viongozi kadhaa wa Kiarabu huko Mashariki ya Kati huku mivutano ya kikanda ikiongezeka kuhusiana na vita vya Israel na Hamas. Katika hatua tofauti Israel imeeleza bayana Jumapili kwamba hakuna Mpalestina ambaye atalazimishwa kuishi nje ya Gaza lakini kwamba vita vitaendelea. Agenda ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken ilijaa mikutano ya ngazi ya juu katika dunia ya Kiarabu jana Jumapili kama sehemu ya juhudi zake za kupunguza mivutano na kuzuia kuenea kwa vita vya Israel na Hamas. Mzozo wa karibuni ulianza wakati Hamas ilipofanya uvamizi wa kigaidi ndani ya eneo la Israel hapo Oktoba 7, na kuua takriban watu 1,200 na kuwachukua mateka watu 240.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #marekani #blinken #biden #hamas #gaza #israel

1/8/2024, 8:56:51 PM

Israel imesema Jumatatu kwamba vikosi vyake vimefanya mashambulizi mapya dhidi ya wanamgambo wa Hamas, katikati na kusini mwa Gaza, pamoja na mashambulizi ya anga dhidi ya kundi la Hezbollah kusini mwa Lebanon.⁣ Mashambulizi hayo yametokea wakati maafisa wa Israel wakisubiri ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, ambaye amesema kwamba ataiomba Israel ijiepushe na mauaji ya raia kwenye operesheni zake huko Gaza, pamoja na kufanikisha upelekeji misaada kwa raia wa Palestina.⁣ Blinken pia ameelezea wasi wasi wake kuhusu uwezekano wa kusambaa kieneo kwa ghasia hizo. “Huu ni mzozo unaoweza kuenea na kusababisha ukosefu zaidi wa usalama, pamoja na mateso,” Blinken amesema Jumapili. Hata hivyo waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameapa kuendelea na mapigano, wakati akiwa kwenye kikao cha kila wiki na baraza lake la mawaziri hapo Jumapili.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #hezbollah #israel #jamas #marekani #blinken

1/8/2024, 8:51:20 PM

Mkuu wa kanisa Katoliki Papa Francis Jumatatu ameomba kupigwa marufuku kote ulimwenguni kwa kile alichokiita visa vya “kuchukiza” vya mtu kubebewa mimba. Papa Francis alisema hayo wakati akijumuisha suala la biashara ya ujauzito, kwenye hotuba yake ya kila mwaka, iliyoangazia tishio lililopo kwa amani ya dunia, pamoja na hadhi ya binadamu. Wakati wa hotuba ya sera za mambo ya nje kwa mabalozi waliopo Vatican, Francis amelalamika kwamba mwaka 2024 umeanza wakati amani ikiwa imetishiwa, kudhoofishwa au hata katika baadhi ya sehemu, kupotea kabisa. Akiangazia vita vya Russia na Ukraine, Israel na Hamas, uhamiaji, mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na utengenezaji haramu wa silaha za nyuklia na silaha nyingine hatari.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #papa #vatican #wanawake #mimba #haki #russia

1/8/2024, 8:46:44 PM

Wizara ya sheria ya Afrika Kusini imesema siku ya Ijumaa kuwa inafungua tena uchunguzi kwa mauaji ya wanaharakati wanne wapinga ubaguzi, moja ya kosa mbaya sana ya uhalifu, lakini halijatatuliwa kwa takriban miongo minne. Wanaharakati hao wanne waliokuwa wakiitwa Cradock Four walitekwa na kuuawa wakati walipokuwa wakijerea nyumbani eneo la Kusini mwa mji wa Cradock mwezi Juni 1985 baada ya mkutano. Miili ya wanaharakati hao wanne-- Matthew Goniwe, Sparrow Mkonto, Fort Calata na Sicelo Mhlauli—iligundulika baada ya siku kadhaa, ikiwa imeungua vibaya na ikiwa na majeraha ya kuchomwa visu. Vikosi vya usalama chini ya utawala wa kibaguzi vinashukiwa kuhusika na mauaji hayo. Lakini hakuna hata mmoja aliyechukuliwa hatua za kisheria. Uchunguzi umefanyika mara mbili—mwaka 1987 na 1993—lakini uchunguzi huo ulizua maswali zaidi kuliko majibu”⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #afrikakusini #ubaguzi #usawa #haki

1/5/2024, 7:41:00 PM

Wafanyakazi 11 wa mgodi wamekwama kwenye chini ya ardhi baada ya kuanguka kwa udongo kwenye Mgodi wa Redwing nchini Zimbabwe, kilomita 270 Magharibi mwa mji mkuu Harare, mamlaka zimesema siku ya Ijumaa. Ajali hiyo imetokea Alhamisi asubuhi, wakati tathmini za awali zikionyesha tetemeko la ardhi ndiyo chanzo cha ajali hiyo, wizara ya madini ya Zimbabwe ilisema katika taarifa yake. Shirika la Metallon, ambalo linamiliki mgodi wa Redwing, lilithibitisha tukio hilo katika taarifa tofauti. Kampuni hiyo imetuma timu ya uokoaji kuwaokoa wachimbaji walionasa na kuwaleta juu ya ardhi, iliongeza.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #zimbabwe #madini #wachimbaji #harare

1/5/2024, 7:09:12 PM

Mwanariadha wa zamani wa Afrika Kusini Oscar Pistorius atolewa gerezani kwa msamaha siku ya Ijumaa na “sasa yuko nyumbani” mamlaka imesema, ni takriban miaka 11 baada ya kumuua kwa kumpiga risasi mpenzi wake Reeva Steenkamp katika uhalifu ulioshtua dunia. Akiwa ametumikia zaidi ya nusu ya kifungo chake, Pistorius mwenye umri wa miaka 37 aliyekatwa viungo viwili aliondolewa kimya kimya kutoka gereza la Atteridgeville lililoko nje kidogo ya mji mkuu Pretoria, kukwepa vyombo vya habari na umati wa watu uliokusanyika nje. Pistorius anayejulikana kama "Blade Runner" kutokana na miguu yake ya bandia, masharti ya kuachiwa kwake ni pamoja na kutozungumza na vyombo vya habari na kukaa ndani ya wilaya ya Waterkloof iliyoko katika jimbo la Pretoria, ambako mjomba wake anaishi, hata hivyo habari kamili kuhusu wapi atakuwa akiishi hazijathibitishwa.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #bladerunner #afrikakusini #pistorius #jela

1/5/2024, 7:02:13 PM

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, anaelekea Mashariki ya Kati huku kukiwa na juhudi kubwa za kidiplomasia ili kuhakikisha ufikishaji wa misaada ya kibinadamu huko Ukanda wa Gaza iliyokumbwa na vita, huku kukiwa na shinikizo la kimataifa kwa Israel kupunguza vifo vya raia wa Palestina. Hii ni ziara ya nne ya Blinken, Mashariki ya Kati toka shambulizi la Oktoba 7 la Hamas dhidi ya Israel na kusababisha vita vinavyo karibia kumaliza mwezi wa tatu. Hamas inachukuliwa kama taasisi ya kigaidi na Marekani, Uingereza, Umoja wa Ulaya na mataifa mengine.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #marekani #israel #gaza #blinken #hamas

1/5/2024, 6:55:14 PM

Rais wa Kenya William Ruto amezua hasira baada ya kuwashutumu baadhi ya watumishi wa mahakama kuchukua rushwa kazini wakati wapinzani wake wakijaribu kuzuia baadhi ya sera za serikali. Rais Ruro ambaye alichaguliwa mwaka 2022, kwa ahadi ya kupunguza ugumu wa maisha kwa Wakenya wa kawaida, ilikuwa ni kampeni yake ya kupunguza deni la taifa, na “matumizi mabaya” ya serikali katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki yenye watu wapatao milioni 53. Mipango kadhaa ya kodi na mpango wa ubinafsishaji uliozinduliwa na serikali kwa ajili ya kufanya mageuzi mbali mbali ya kiuchumi imezuiliwa na mahakama baada ya changamoto za kisheria mwaka jana.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #kenya #ruto #mahakama #rushwa

1/4/2024, 9:16:17 PM

Mahakama ya juu ya Umoja wa Mataifa itasikiliza shauri la Afrika Kusini, na Israel, wiki ijayo baada ya Pretoria kufungua kesi kwa kile ilichokiita mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza. Afrika Kusini inaitaka Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuiamuru Israel kusitisha operesheni zake za kijeshi huko Gaza, katika kesi ambayo Israel imeipinga na kukasirishwa. Marekani, Jumatano iliikosoa Afrika Kusini, kwa kuwasilisha kesi ya mauaji ya kimbari, na kupinga shutuma dhidi ya Israel kuhusu vita vyake huko Gaza. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Matthew Miller amesema kwamba kutokana na tathmini ya Marekani, “hatujaona vitendo vinavyojumuisha mauaji ya kimbari kwa wakati huu.” •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #un #afrikakusini #israel #mahakama⁣ ⁣ ⁣ ⁣

1/4/2024, 5:19:36 PM

Maafisa wa NATO na Ukraine wanatazamiwa kukutana wiki ijayo kujadili mashambulizi ya anga yanayofanywa na Russia dhidi ya Ukraine, yakiwa ni pamoja na wimbi kubwa la mashambulizi, ambayo yamefanyika tangu mwaka huu kuanza. Msemaji wa NATO Dylan White alisema Alhamisi kwamba Katibu Mkuu wa Shirika hilo, Jens Stoltenberg ataitisha kikao cha Baraza la NATO, kujadili vita vya Ukraine, hapo Januari 10, "kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni ya makombora ya Russia, pamoja na yale ya ndege zisizo na rubani."⁣ Maafisa wa Ukraine wameshinikiza washirika kuimarisha ulinzi wa anga wa nchi hiyo, huku Russia ikitumia makombora na ndege zisizo na rubani, kila siku, kulenga miji ya Ukraine.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #nato #ukraine #russia #vita #droni #marekani #qatar

1/4/2024, 5:14:24 PM

Zambia inatarajiwa kukubaliana juu ya masharti muhimu ya kufanyia marekebisho ya mikopo yake ya jumla ya dola bilioni 3 za Marekani, kabla ya robo ya kwanza ya mwaka 2024, waziri wa fedha wa nchi hiyo Felix Nkulukusa alisema Alhamisi. Nchi zinazodaiwa, zinatarajiwa kukubaliana na mikataba ya urekebishaji linganishi, na wakopeshaji rasmi, na wale wa kibiashara, chini ya mchakato wa Mfumo wa Pamoja wa G20, ambao ulianzishwa mnamo mwaka 2020, ili kukabiliana na athari za janga la COVID-19. Katika kile kinachoonekana kuwa kikwazo kikubwa kwa Zambia, wakopeshaji wake rasmi, ambao ni pamoja na China na wanachama wa Klabu cha Paris, cha mataifa yanayotoa mikopo ya kimataifa, walikataa mpango wa awali wa marekebisho ya mikopo, hapo mwezi Novemba mwaka jana.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #zambia #marekani #deni #mikopo #g20 #china

1/4/2024, 5:04:50 PM

Sierra Leone siku ya Jumatano imemfungulia mashitaka ya uhaini pamoja na makosa mengine Rais wa zamani wa nchi hiyo Ernest Bai Koroma kwa kile mamlaka ilichodai jukumu lake katika jaribio la mapinduzi la Novemba 26, Mamlaka imesema. Korona ambaye aliliongoza taifa hilo la Afrika Magharibi kuanzia 2007 hadi 2018, awali alihojiwa, mamlaka ikisema alikuwa mshukiwa rasmi katika mipango ya mapinduzi. “Rais huyo wa zamani ameshitakiwa kwa makosa manne yakiwemo uhaini, makossa ya uhaini na kwa mashitaka mawili ya kuhifadhi,” taarifa iliyosainiwa na waziri wa habari Chernor Bah imesema.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #sierraleonne #koroma #jeshi #mapinduzi #niger #mali

1/3/2024, 8:26:30 PM

Mchungaji mashuhuri wa Uganda na ambaye pia ni muungaji mkono sugu wa rais wa Uganda Yoweri Museveni amelazwa hospitali baada ya shambulizi la bunduki ambalo lilimuuwa mlinzi wake, polisi wamesema leo Jumatano. Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, mchungaji Aloysius Bugingo alipigwa risasi Jumanne jioni baada ya watu wasiojulikana kushambulia gari lake, na kisha kutoroka kwa kutumia pikipiki mjini Kampala, ripoti imeongeza. Muhoozi Kainerugaba ambaye ni mtoto wa kiume wa Museveni na huenda akawa mrithi wa baba yake, amesema kwamba alizungumza na “mfuasi wao sugu” Bugingo, na kwamba yupo sawa.“Alipata majeruhi madogo kwenye bega lake la kushoto,” ameongeza kusema kupitia ukurasa wake wa X, akilitaja tukio hilo kuwa la “kikatili.’ Bugingo ni mmoja wa watu mashuhuri wenye utata nchini Uganda, ni kiongozi wa kanisa la House of Prayer Ministries, moja ya makanisa ya kipentekoste, lenye ushawishi mkubwa zaidi kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki. Bugingo pia anamiliki vituo vya televisheni na radio, ambavyo huvitumia kumuunga mkono Museveni ambaye ametawala Uganda tangu 1986.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #uganda #museveni #bugingo #kainerugaba

1/3/2024, 5:38:45 PM

Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema Jumatano kwamba mfumo wake wa ulinzi umeharibu makombora 12 ya Ukraine yaliyorushwa kwenye mkoa wa Belgorod, siku chache baada ya shambulizi la Ukraine katika eneo hilo kuuwa watu 21 na kupelekea ahadi kutoka kwa rais wa Russia Vladimir Putin ya kuongezwa kwa mashambulizi. Jumanne ilikuwa ni siku ya ongezeko la mashambulizi ya Russia yaliyoua takriban watu watano na kujeruhi wengine karibu 130 huko Kyiv na Kharkiv, maafisa wa Ukraine wamesema. Jeshi la anga la Ukraine limesema kwamba vikosi vya Russia vilitumia droni 35 na makombora 99 kutoka angani na kwenye bahari, na kwamba ulinzi wa Ukraine uliangusha droni zote pamoja na makombora 72. Waziri wa mambo ya nje wa Poland Radoslaw Sikorski amesema mapema leo kwamba kutokana na ongezeko la mashambulizi dhidi ya Ukraine, washirika wake wanahitaji kuongeza vikwazo kwa Russia, pamoja na kutoa silaha za masafa marefu kwa vikosi vya Ukraine.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #russia #ukraine #putin #zelenskyy #vita

1/3/2024, 5:23:31 PM

Waziri mkuu wa Nigeria ameungana na mawaziri wakuu wenzake wa nchi jirani zinazoongozwa na jeshi za Mali na Burkina Faso kuangalia mashindano ya mieleka yaliyofanyika Niger, katika mji wa kaskazini wa Agadez.⁣ Katika tukio hilo ambapo mshindi “Issaka Issaka” alidondoka kwa kupiga magoti, mikono ameinyanyua kwa shangwe. Baada ya dakika nane tu, mpinzani wake alipiga magoti na kuinamisha kichwa kugusa mchanga, hivyo kumpa ufalme wa mchezo “Issaka Issaka” katika ushindi wa kihistoria Hivi sasa ni mwaka wa 44, wa tukio hilo la kitaifa la Saber kwa ujumbe wa hivi sasa “ulinzi wa nyumbani.” ⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #junta #burkinafaso #mali #niger

1/2/2024, 6:34:48 PM

Mashambulizi mazito ya makombora na ndege zisizokuwa na rubani huko Kyiv na mji wa Kaskazini Mashariki mwa Kharkiv yameuwa raia wawili na kujeruhi darzeni wengine na kusababisha uharibifu katika meneo hayo, maafisa wa Ukraine wamesema. Russia imeshambulia kwa kutumia makombora tofauti wakati wa majira ya asubuhi yaliyokuwa na harakati nyingi, wakipiga majengo ya wakaazi, na miundombinu. Mamlaka za jeshi zilitoa onyo la mashambulizi ya anga ambayo yalidumu kwa saa tatu. Shambulizi limekuja saa kadhaa baada ya rais wa Russia Vladmir Putin kusema shambulizi la anga katika mji wa Russia – Belgorod, halitapita bila kuadhibiwa. Moscow imesema shambulizi la anga limeuwa raia 24 na kuilaumu Ukraine. ⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #kyiv #russia #moscow #putin #russia

1/2/2024, 6:16:09 PM

Israeli ilifanya mashambulizi ya anga kote katika Ukanda wa Gaza siku ya Jumanne, huku wakazi wakiripoti mapigano makali kati ya wanajeshi wa Israeli na wanamgambo wa Hamas katikati na kusini mwa Gaza. Mapigano ya Jumanne yalijumuisha eneo la Al-Bureij katikati mwa eneo la Wapalestina na Khan Younis, mji wa kusini ambao ni wa pili kwa ukubwa, katika Ukanda wa Gaza. Jeshi la Israeli pia lilisema limefanya mashambulizi mapya ya anga kusini mwa Lebanon, yakilenga wanamgambo wa Hezbollah, washirika wa Hamas ambao wamekuwa wakikabiliana na wanajeshi wa Israeli, tangu vita kuanza huko Gaza. Shirika la habari la serikali ya Syria limesema mashambulizi kadhaa ya anga ya Israeli yalilenga viunga vya Damascus na kusababisha "uharibifu wa mali." ⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #hamas #israel #gaza #khanyounis

1/2/2024, 5:48:53 PM

Watu wasiopungua watano wamepoteza maisha baada ya ndege ya abiria ya Japan kushika moto siku ya Jumanne usiku wakati ikishuka kwenye barabara ya uwanja wa ndege wa Haneda mjini Tokyo, baada ya kugongana na ndege nyingine ya walinzi wa pwani. Ripoti zinasema kuwa abiria na wana hewa wote walitolewa kwenye ndege hiyo iliyokuwa ikiwaka moto. Picha za televisheni zilionyesha miali ya moto ikitokea kwenye madirisha na sehemu ya ndani ya ndege ya shirika la ndege la Japan Airlines wakati wafanyakazi wa zima moto wakipambana na moto huo. Vyombo vya habari vya Japan viliripoti kuwa ndege hiyo ilitua katika uwanja wa Haneda ikitokea kwa uwanja wa ndege wa Shin-Chitose huko Hokkaido, zaidi ya kilomita 1,200 kaskazini mwa Tokyo, ikiwa na abiria 379 na pamoja na wafanyakazi. Vyombo vya habari viliripoti kuwa wafanyakazi watano kati ya sita waliokuwa kwenye ndege ya walinzi wa pwani wamethibitishwa kufariki.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #japani #ndege #ajali #ulinzi

1/2/2024, 5:44:08 PM

Mashambulizi ya anga Mashariki mwa Syria, ambayo yanadhaniwa kufanywa na Israel, yameua wapiganaji 23 wanaoungwa mkono na Iran, siku ya Jumamosi, waangalizi wa vita wameripoti vifo zaidi vinne Kaskazini mwa nchi hiyo . Kundi la uangalizi wa haki za binadamu, limesema wapiganaji 23 wanaoiunga mkono Iran, ikijumuisha raia wa tano wa Syria, wanne kutoka kundi la Hezbollah la Lebanon, raia sita wa Iraq, na wanane wa Iran waliuwawa katika mashambulizi tisa ya anga karibu na mpaka wa Iraq. Imesema mashambulizi hayo kuna uwezekano yamefanywa na Israel, baada ya hapo awali kuelezwa kuwa kuna uwezekano yalifanywa na Marekani. Afisa wa jeshi la Marekani ambaye hakutaka kutambulishwa amesema Marekani, haikufanya mashambulizi yoyote nyakati za usiku. Kundi hilo limesema mashambulizi yalilenga maeneo ya Albu Kamal, na mengine yanayozunguka jimbo la Deir el-Zour.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #syria #iran #ukraine #russia #hezbollah #hamas

1/1/2024, 8:46:56 PM

Mahakama za Russia, zimewahukumu zaidi ya wapiganaji 200 wa Ukraine, kwenda gerezani tangu Moscow, ilipoanza opereshini zake za kijeshi nchini Ukraine, amesema waziri wa mambo ya nje Sergei Lavrov katika mahojiano na shirika la habari la RIA, Jumapili. Lavrov ameiambia RIA kwamba mahakama za Russia zimewahukumu zaidi ya wawakilishi 200 wa jeshi la Ukraine, kwa kvitendo vya unyama. Pande zote zinashutumiana kwa kufanya unyama katika vita ambavyo vimeanzishwa na Russia baada ya kuivamia Ukraine, Febuari 2022. Umoja wa Mataifa unaendelea kupata ushahidi wa uhalifu wa kivita, na uvunjifu wa haki za binadamu uliofanywa na serekali ya Russia, ikijumuisha mateso, ubakaji, na usafirishaji wa watoto.⁣ Mwezi Machi, mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC ilitoa hati ya kukamatwa kwa rais wa Russia, Vladimir Putin, kwa usafirishaji wa watoto kuwa umefikia kiwango cha uhalifu wa kivita.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #russia #moscow #ukraine #vita

1/1/2024, 8:40:57 PM

Wanamgambo wa Hamas katika Ukanda wa Gaza walirusha msururu wa roketi siku ya Jumatatu, na kusababisha ving'ora vya mashambulizi kusikika maeneo mbalimbali za Israel. Hakuna taarifa zozote za uharibifu au vifo kutoka kwenye roketi hizo, ambazo Hamas imeendelea kuzitumia kuilenga Israel huku wanajeshi wa Israel wakifanya mashambulizi ya kuwaondoa Hamas huko Gaza. Mashambulizi ya Israel huko Gaza yaliendelea siku ya Jumatatu kwa operesheni za ardhini na mashambulizi ya anga, ikiwa ni pamoja na kile Jeshi la Ulinzi la Israel lilisema ni shambulio lililomuua kamanda wa Hamas ambaye alisaidia kuwaongoza wapiganaji waliohusika na shambulio la kigaidi la Oktoba 7 kusini mwa Israel.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #hamas #israel #gaza #misri #qatar #jesi #ulinzi

1/1/2024, 8:33:59 PM

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un ameapa kuzindua satelaiti za ujasusi za kijeshi, kuzalisha zaidi vifaa vya nyuklia, na kuzindua ndege zisizo na rubani za mashambulizi kwa mwaka 2024. Alielezea wakati akizungumzia utayari wa kivita ili kukabiliana na hatua za kichokozi za Marekani, vimeripoti vyombo vya habari vya serikali siku ya Jumapili. Kiongozi huyo alitoa kauli hizo wakati wa mkutano wa chama cha wafanyakazi ambacho kilijiwekea malengo kwa mwaka huu na kueleza kuongeza majaribo ya silaha kabla ya uchaguzi wa Novemba wa Marekani. Waangalizi wanasema Kim anaamini katika kuongeza uwezo wa silaha za nyuklia na kumpatia fursa nyingine kubwa ya kidiplomasia na Marekani, ili apate afueni ya vikwazo kama Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump atarejea madarakani.⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #koreakaskazini #ujasusi #kimjongun #marekani

1/1/2024, 8:15:26 PM

Siku ya mwaka mpya ilianza hapa Marekani kwa maelfu ya watu kukusanyika katika uwanja wa Times Square mjini New York , ambapo mpira wa kioo unaong’aa ulianza kushuka pole pole kuashiria kuingia kwa mwaka 2024 kwa matumaini licha ya kuwepo migogoro inayoendelea duniani.⁣ Kulikuwa na picha zinazoonyesha furaha katika nchi mbali mbali wakati mwaka mpya ulipokaribishwa kwa matumaini kwamba siku zinazofuata zitaleta furaha zaidi kuliko huzuni⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #mwakampya #marekani #newyork

1/1/2024, 5:28:32 PM

Mamlaka ya Uturuki zimewashikilia watu 29 wanaotuhumiwa kuwa na ushirikiano na kundi la wanamgambo la Islamic state katika operesheni kwenye majimbo tisa ikiwemo Instanbul na Ankara, waziri wa mambo ya ndani Ali Yerlikaya alisema siku ya Ijumaa. Kufuatia vyanzo vya usalama shirika la habari la uturuki Anadolu limesema kwamba watuhumiwa wengine watatu wanaohusishwa na watu 29 walioshikiliwa wamekamatwa katika operesheni hiyo pia. Imesema watatu hao walikuwa wanachama wa juu wa kundi la Islamic state, na kuongeza kuwa mmoja alipanga shambulizi katika ubalozi wa Iraq mjini Ankara. Watuhumiwa walikamatwa katika operesheni zinazojulikana kama “heroes 37” zilizofanyika Ijumaa ambapo taarifa zilikusanywa katika makanisa na mahekalu mjini Instanbul, alisema Yerlikaya kupitia mtandao wa kijamii wa X akiongeza kuwa maeneo mengine 39 yalivamiwa. ⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ •⁣ #voa #voaswahili #africa #uturuki #islamicstate #jihadi #iraq

12/29/2023, 6:08:38 PM